Vinega au Siki
Apple cider siki na vinega nyeupe, hupunguza harufu kwapani. Ili kukabiliana na harufu, loweka pamba katika vinega, paka kwenye makwapa badala ya deodorant. Mbali na tiba hiyo, tumia tea tree oil, inaweza pia kuwa na manufaa kwa sababu ni anti-bacterial.
Limao
Kata limao au ndimu nusu kwa kisu. Paka kipande cha limao ulichokata kwenye kwapa lako na hakikisha unalisugua mpaka litoe maji yake. Weka kwapa lako lipate hewa ili hiyo juice ya limao uliyopaka ikauke.
Asidi citric katika maji ya limao inasaidia kutoa tezi ya jasho hivyo kuondoa harufu.