Kuna mambo mengi ya kiasili ambayo wengi hatuyajui na mojawapo ni Mvua ya Samaki.
Najua sio rahisi kuamini lakini ukweli ni kwamba lipo na uwepo wake umewahi kuripotiwa katika nchi mbalimbali ulimwenguni.
Hii ni nini hasa?
Ni moja kati ya matukio adimu ya ki - Hali ya Hewa, ambapo wanyama walioruka kama samaki na chura wana "Nyesha" kutoka angani. Wana sayansi wanasema hii hutokea pale upepo mkali unapopita kwenye vyanzo vya maji na kubeba viumbe kama samaki na chura na kwenda kuanguka sehemu nyingine.
