Tuesday, November 26, 2013

MWANAMKE MWENYE KIPAJI CHA KUCHORA SURA ZA WATU ASIOWAJUA; HUTUMIWA KUKAMATA WAHALIFU MAREKANI















Kazi ya kuchora taswira ya mhalifu ni hatua kubwa na ngumu kwa polisi katika uchunguzi, lakini sivyo ilivyo kwa LOIS GIBSON.
Kipaji chake kimempa nafasi ya kuvunja rekodi ya dunia ya Guiness ya mchoraji maarufu zaidi.
Kwa muda wa uzoefu wake wa miaka 30, Lois amefanikiwa kukamatisha zaidi ya wahalifu 1000. Zoezi hili linashangaza zaidi kwa kuzingatia kuwa yeye huchora taswira hizo bila kuwaona wahalifu hao, na wala hajawahi kuwaona kabla, isipokua huchora kwa kusikiliza maelezo ya waathirika wa matukio ya uhalifu. 
Akiwa na umri wa miaka 21, Lois aliwahi kuvamiwa na kupigwa karibu na kufa, sababu iliyompelekea kuanza uchoraji wa wahalifu. Alianza kama mchoraji wa mtaani, na baadaye kujitolea kuchora kwa kuisaidia polisi. Baada ya picha mbili kutofanikiwa, picha ya tatu ilifanikiwa kukamatisha mhalifu na amekuwa akitumiwa na polisi  kwenye matukio mengi.
Katika picha hapo juu ni baadhi ya taswira alizowahi kuchora, na jinsi gani zinavyofanana na wahusika