Monday, December 2, 2013

MWANAMAMA ANAYEFANYA MAZOEZI YA KUNYANYUA VITU VIZITO HADI WIKI 2 KABLA YA KUJIFUNGUA



Kwa mimba ya miezi 8 na wiki 2 ni kawaida kwa wanawake wengi kupumzika, Lakini imekua tofauti sana kwa Lea Ellison. Mama huyu ambaye mpaka wiki mbili tu kabla ya kujifungua kwake bado amekuwa akifanya mazoezi ya viungo yafanywayo haswa na wataalam wa mbio na wanajeshi
Lea-Ann Ellison amesema kuwa amekuwa akifanya mazoezi hayo ya kunyanyua vitu vizito tangu akiwa na miaka 16, na kuacha kufanya hivyo sababu ya mimba kubwa, atakuwa hautendei haki mwili wake. 
Lea-Ann anayetegemea kupata mtoto wake wa tatu, akiwa na umri wa miaka 35, amejikuta akiingia katika upinzani wa hali ya juu baada ya picha yake akinyanyua vyuma kuonekana katika mtandao wa kijamii 'Facebook', ambapo watu wamedai kuwa kubeba uzito mkubwa huweza kumsababishia mimba kutoka au kuharibika. 
Hata hivyo mwanamama huyo kutoka Los Angeles hajachukizwa hata kidogo na maoni ya watu, lakini amesema hangeweza kufanya kitu chochote kilicho hatari kwa mtoto wake. Uzito anaonyanyua ni mdogo sana (paundi 45 na si 145 kama wana mazoezi wengine). Kwake Lea, ujauzito si ugonjwa bali ni wakati wa kufurahia mwili wake.