Saturday, March 15, 2014

Daima mshukuru Mungu kukuumba Mzima, tizama hawa wenye miguu ya ajabu.


Vadoma ni kabila la watu wanaoishi vijiji vya Maghalibi mwa mchi ya Zimbabwe. Watu hawa wamepewa jina la utani la "Ostrich people" yaani "Watu-mbuni". (Mbuni ni ndege mwenye vidole viwili). Watu wa vadoma wana kabiliwa na tatizo la kimaumbile lijulikanalo kama Ectrodactyly, ambapo watoto huzaliwa wakiwa na vidole viwili tu miguuni kama inavyoonekana kwenye picha. Ugonjwa huo unaweza kuathiri aidha mikono au miguu.

Ectrodactyly ni ugonjwa wa kurithi kutoka kizazi hadi kizazi. Baadhi ya watu wa jamii hiyo huchukulia tatizo hilo kama faida kwani huwasaidia katika kukwea miti. Tatizo hilo limeonekana kuwapata watu wa jamii ya vadoma pekee kwani mila na desturi zao hazimruhusu mtu kuoa nje ya jamii/kabila hilo.

Share na U-Like Habari hii kumshukuru Mungu kwa kukuumba kama mkamilifu.