Friday, March 21, 2014
Mambo 7 ya kufanya ili Kudumisha Mapenzi kwenye Ndoa
Wanandoa wengi hulalamika kwamba Ndoa zao zimepoteza mvuto na mahaba yaliokuwepo toka mwanzo. Watu wengi huamini kwamba Ndoa haina changamoto nyingi. Kutokana na ubize wa maisha na shughuli za kila siku mara nyingi tunakosa mda wa kukaa na wapenzi wetu, jambo ambalo hupelekea kutoelewana ndani ya nyumba na pia huondoa mahaba. Kwa kawaida ni mambo madogo madogo ndio yanasababisha magomvi katika mapenzi na hata kuvunjika kwa ndoa.
Watafiti wanasema kila Ndoa hupitia hatua 3 kuu:
1. Mahaba mazito: Hatua hii ni kile kipindi cha mwanzo katika ndoa. Katika hatua hii wanandoa au wapenzi hutumia muda mwingi kuambiana kuhusu hisia.
2. Marekebisho: Katika hatua hii ndipo matatizo madogo madogo huanza kujitokeza. Kipindi hiki mabishano hua mengi na maranyingine hata mapigano. Kila mmoja anakua anajiona yupo sahihi. Ndoa nyingi huvunjika katika hatua hii.
3. Kujito / Kujikomit: Katika hatua hii wanandoa huamua kujitoa kwaajili ya wapenzi wao. Kwenye hatua hii mabishano hupungua kwa kiasi kikubwa na kila mmoja huamua kukubaliana na mapungufu ya mwenzake.
Pamoja na hayo, zipo njia au mambo ya kufanya ili kurejesha mvuto wa kimahaba kwenye Ndoa yako:
1. Kupeana zawadi: Kupeana zawadi husaidia kukumbushana siku za mwanzo wa mapenzi yenu ambayo humfanya mpenzi wako kua karibu zaidi na wewe. Zawadi ziwe ni kitu chochote ambacho kitakukumbusha nyakati muhimu katika mapenzi yenu kama Mlipokutana kwa mara ya kwanza.
2. Mshirikishe mpenzi wako katika Maamuzi Muhimu: Hii itakusaidia kumfanya mpenzi wako aone jinsi unavyo mthamini. Pia itamfanya ajiamini zaidi, jambo ambalo hupelekea mtu kujisikia vizuri, na unapojisikia vizuri unapenda zaidi.
3. Mawasiliano: Mawasiliano ni jambo muhimu sana katika ndoa. Msiache kutumiana meseji za kimahaba na mapenzi. Daima mjulishe mpenzi wako kuhusu hisia zako, mabadiliko yoyote na kila unapotoka kwenda mahali na kama utachelewa kurudi.
4. Msifie: Watu wengi hupenda kusifiwa, lakini sifa huwa inakua ya muhimu zaidi kama inatoka kwa mpenzi wako. Kamwe usisahau kumwambia mpenzi wako kila unapoona amependeza. Msifie pia kuhusu mambo mengine kama malezi, kupika na kuijali familia. Unapoonyesha kuridhishwa na kufurahishwa na mambo ya mpenzi wako, unamfanya ajisikie kupendwa jambo ambalo hudumisha muungano wenu.
5. Mambo madogo madogo: Unapofanya mambo madogo madogo kama kumbusu mpenzio kabla ya kwenda kazini, huweka tofauti kubwa sana kwenye ndoa. Mambo kama haya hayahitaji jitihada kubwa lakini husaidia sana kuimarisha mahaba kwenye ndoa.
6. Tumia muda kukaa na Mpenzio: Ni muhimu sana kutenga muda wa kufurahia pamoja na mpenzi wako. Tafuta hata filamu iliyokaa kimahaba na uangalie pamoja na mpenzi wako.
7. Jaribu kufurahia kitu anachopenda: Kila siku jaribu kufurahi na mpenzi wako katika kile kitu au jambo analolipenda. Kama ni kucheza Game pamoja, kwenda disko pamoja, kuangalia mpira pamoja na mambo kama hayo.
Kama unakubaliana na Dondoo hizi muhimu, usisite ku-Share na wenzako kwa kubonyeza vitufe hapo chini
