Saturday, April 12, 2014
Sunday, April 6, 2014
Mambo 5 utakayo kutana nayo katika safari ya Kufanikisha Ndoto zako
1. Utapitia wakati mgumu. Utatoka katika eneo lako la Faraja (Comfort zone).
Lakini baadaye mambo yatakaa sawa na utarudi kwenye eneo lako la faraja
2. Utaogopa.
Mara nyingine utapatwa na woga wa kufeli katika jambo unalolifanya, lakini baadaye utazoea na woga utaisha.
3. Saa nyingine utakua hauna uhakika na kile unachokifanya.
Wakati hauna uhakika unatakiwa uamue cha kufanya kati ya haya:
i. Kuachana na kile ukifanyacho na kisha kusubiria msukumo mwingine uje ukupeleke kwenye hatua inayofata. AU
ii. Kuchukua hatua ya imani na kufanya bila kujali, huku ukijua kwamba hata kama uamuzi wako utakua siyo sahihi, maisha yataendelea na utakua umejifunza kitu muhimu katika safari yako ya mafanikio.
4. Utashawishika kuacha na kujaribu kufanya kitu kingine chenye usalama/uhakika zaidi:
Usikubali kushawishika, hakuna kazi yenye usalama wa uhakika duniani kama unataka kufanikiwa.
5. Hautoweza kumfurahisha kila mtu.
Daima kutakua na watu ambao hawafurahishwi na kile unachokifanya, na kwa bahati mbaya baadhi yao wanaweza kua ni watu wa karibu yako na unao wajali. Sio tatizo; wewe funga mdoma wako na uendelee na mipango ya kufanikisha Ndoto zako bila kusubiria wakukubali. Mda sio mrefu utaanza kuona watu wanajitokeza kuungana mkono na wewe.
Wednesday, April 2, 2014
Mwanaume ajaribu kujizika kukwepa matatizo ya ndoa Kenya
Mwanamume mmoja nchini Kenya aliwaacha wakazi wa kijiji cha Tivani mkoa wa Bonde la uffa vinywa wazi baada ya kujichimbia kaburi na hata kujaribu kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni matatizo ya ndoa.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha KTN nchini Kenya, tukio hilo lililotokea Jumanne asubuhi na kuwashangaza wakazi wa eneo la Trans Nzoia mkoa wa Rift Valley
Mwanamume huyo, alidai kuwa ana matatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe ameshidwa kuyatatua na kwa hivyo kwake kilichosalia ni kwenda mbinguni.
Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndhio maana akaamua kujitoa uhai.
Mwanamume huyo kwa jina Kipsang , alichimba kaburi hilo usiku na hata kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na watoto wake walipokuwa wanalala.
Wanakijiji katika kijiji cha Tivani walikuwa na wasiwasi kuwa mwanamume huyo alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri kwamba yeye na mkewe wamekuwa wakikumwba na matatizo ya ndoa.
Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake.
Baba huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa matatu, hatimaye aliondoka katika kaburi hilo baada ya wanakijiji kumsihi huku wazee wakiwataka watu kupanda migomba ya Ndizi neneo alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi.
Chanzo: BBC
Labels:
afya ya akili,
Maajabu,
maisha,
saikolojia,
vioja,
Vituko
Tuesday, April 1, 2014
Mtoto wa miaka 2 aokoa maisha ya mamake
Mtoto mwenye umri wa miaka miwili nchini Uingereza Riley Ward amepokea sifa kedekede kwa kuokoa maisha ya mamake kwa kupiga nambari ya simu 999 baada ya mamake kuzimia.
Wahudumu wa afya katika kituo cha kupokea simu za dharura nchini Uingereza walisema kuwa walipokea simu ya mtoto mdogo aliyewambia ''Mama amelala''
Wahudumu hao walifanikiwa kwenda nyumbani kwa mtoto huyo katika mtaa Leicestershire, na kumpa huduma ya kwanza mamake mtoto huyo na kisha kumpeleka hospitalini.
Walimfanyia upasuaji wa dharura baada ya kupatikana na damu iliyokuwa imeganda kichwani huku akivuja damu nyingine kutoka katika kizazi chake.
Sasa mtoto huyo Riley Ward amezawadiwa kwa kitendo chake cha ujasiri na wahudumu hao waliosema kuwa huyo ndiye mtoto mchanga kabisa kuwahi kupiga simu kituoni humo.
Mamake , Dana Henry, alimtaja mwanawe kama shujaa wake mdogo.
Dana mwenye umri wa miaka 27 alisema kuwa alishtushwa sana na kitendo cha mtoto wake aliyekuwa na uwezo wa kupiga simu.
Pia alisema kuwa ameweza kuwafundisha watoto wake wadogo namna ya kupiga simu ya dharura ikiwa yeye na mumewe hawahisi vizuri.
Chanzo: BBC
Friday, March 28, 2014
Madhara ya Uvutaji Sigara kwa kina mama wajawazito watoto wanaozaliwa
Utafiti mpya kutoka ulaya na marekani kazkazini unasema kuwa,kupigwa marufuku kwa uvutaji wa sigara hadharani kumesababisha kushuka kwa viwango vya wanawake kujifungua mapema kabla ya mda wao kwa asilimia 10.
Idadi ya watoto waliolazwa hospitalini kutokana na ugonjwa wa pumu pia imepungua kwa asilimia 10% katika maeneo ambayo uvutaji sigara hadharani umepigwa marufuku kulingana na wanasayansi kutoka chuo cha Edinburgh nchini Scotland.
Mmoja ya waanzilishi wa utafiti huo Prof Aziz Sheikh ambaye ripoti ya utafiti wake imechapishwa katika jarida la matibabu duniani Lancet,anasema kuwa mataifa yasio na marufuku hiyo yanapaswa kutilia maanani matokeo hayo kwaajili ya kizazi chao cha baadaye.
Kwa sasa ,sheria dhidi ya uvutaji sigara zinaathiri asilimia 16 ya idadi ya watu dunaini.
Chanzo: BBC Swahili
Rangi ya Mkojo wako inamaana gani kwa Afya yako? Soma hapa ujue
1. Mweupe kabisa (Usio na Rangi):
Unakunywa maji mengi kupita kiasi. Ikiwezekana unashauriwa upunguze kidogo
2. Manjano iliyochanganyika na Kijani kidogo: Ni kawaida, una afya na Mwili wako una maji ya kutosha.
3. Manjano iliyo pauka:
Upo kawaida tu. Endelea kunywa maji ya kutosha
4. Njano iliyo kolea:
Upo kawaida lakini unashauriwa kunywa maji ya kutosha.
5. Njano inayokaribia kufanana na Kahawia au Rangi kama ya Asali:
Mwili wako hauna maji ya kutosha. Kunywa maji kwa wingi sasa.
6. Rangi ya Kahawia:
Huwenda una Matatizo kwenye Ini lako au Upungufu mkubwa wa Maji mwilini. Kunywa maji ya kutosha na umwone daktari kamali hii ikiendelea.
7. Rangi ya Pinki inayokaribia kuwa kama Nyekundu:
Kama hujala matunda yoyote nyenye asili ya uwekundu, basi huwenda una Damu kwenye kibofu chako cha mkojo. Inaweza ikawa sio ishara mbaya. Lakini inaweza ikawa ishara ya ugojwa wa Figo, uvimbe, matatizo kwenye njia ya mkojo, au matatizo kwenye kibofu. Muone daktari haraka iwezekanavyo.
Kama unadhani Dondoo hii ni Muhimu, Gonga "SHARE" ili kuwajuza na wenzako.
Friday, March 21, 2014
Mambo 7 ya kufanya ili Kudumisha Mapenzi kwenye Ndoa
Wanandoa wengi hulalamika kwamba Ndoa zao zimepoteza mvuto na mahaba yaliokuwepo toka mwanzo. Watu wengi huamini kwamba Ndoa haina changamoto nyingi. Kutokana na ubize wa maisha na shughuli za kila siku mara nyingi tunakosa mda wa kukaa na wapenzi wetu, jambo ambalo hupelekea kutoelewana ndani ya nyumba na pia huondoa mahaba. Kwa kawaida ni mambo madogo madogo ndio yanasababisha magomvi katika mapenzi na hata kuvunjika kwa ndoa.
Watafiti wanasema kila Ndoa hupitia hatua 3 kuu:
1. Mahaba mazito: Hatua hii ni kile kipindi cha mwanzo katika ndoa. Katika hatua hii wanandoa au wapenzi hutumia muda mwingi kuambiana kuhusu hisia.
2. Marekebisho: Katika hatua hii ndipo matatizo madogo madogo huanza kujitokeza. Kipindi hiki mabishano hua mengi na maranyingine hata mapigano. Kila mmoja anakua anajiona yupo sahihi. Ndoa nyingi huvunjika katika hatua hii.
3. Kujito / Kujikomit: Katika hatua hii wanandoa huamua kujitoa kwaajili ya wapenzi wao. Kwenye hatua hii mabishano hupungua kwa kiasi kikubwa na kila mmoja huamua kukubaliana na mapungufu ya mwenzake.
Pamoja na hayo, zipo njia au mambo ya kufanya ili kurejesha mvuto wa kimahaba kwenye Ndoa yako:
1. Kupeana zawadi: Kupeana zawadi husaidia kukumbushana siku za mwanzo wa mapenzi yenu ambayo humfanya mpenzi wako kua karibu zaidi na wewe. Zawadi ziwe ni kitu chochote ambacho kitakukumbusha nyakati muhimu katika mapenzi yenu kama Mlipokutana kwa mara ya kwanza.
2. Mshirikishe mpenzi wako katika Maamuzi Muhimu: Hii itakusaidia kumfanya mpenzi wako aone jinsi unavyo mthamini. Pia itamfanya ajiamini zaidi, jambo ambalo hupelekea mtu kujisikia vizuri, na unapojisikia vizuri unapenda zaidi.
3. Mawasiliano: Mawasiliano ni jambo muhimu sana katika ndoa. Msiache kutumiana meseji za kimahaba na mapenzi. Daima mjulishe mpenzi wako kuhusu hisia zako, mabadiliko yoyote na kila unapotoka kwenda mahali na kama utachelewa kurudi.
4. Msifie: Watu wengi hupenda kusifiwa, lakini sifa huwa inakua ya muhimu zaidi kama inatoka kwa mpenzi wako. Kamwe usisahau kumwambia mpenzi wako kila unapoona amependeza. Msifie pia kuhusu mambo mengine kama malezi, kupika na kuijali familia. Unapoonyesha kuridhishwa na kufurahishwa na mambo ya mpenzi wako, unamfanya ajisikie kupendwa jambo ambalo hudumisha muungano wenu.
5. Mambo madogo madogo: Unapofanya mambo madogo madogo kama kumbusu mpenzio kabla ya kwenda kazini, huweka tofauti kubwa sana kwenye ndoa. Mambo kama haya hayahitaji jitihada kubwa lakini husaidia sana kuimarisha mahaba kwenye ndoa.
6. Tumia muda kukaa na Mpenzio: Ni muhimu sana kutenga muda wa kufurahia pamoja na mpenzi wako. Tafuta hata filamu iliyokaa kimahaba na uangalie pamoja na mpenzi wako.
7. Jaribu kufurahia kitu anachopenda: Kila siku jaribu kufurahi na mpenzi wako katika kile kitu au jambo analolipenda. Kama ni kucheza Game pamoja, kwenda disko pamoja, kuangalia mpira pamoja na mambo kama hayo.
Kama unakubaliana na Dondoo hizi muhimu, usisite ku-Share na wenzako kwa kubonyeza vitufe hapo chini
Subscribe to:
Comments (Atom)









