Tuesday, July 16, 2013

Muujiza - Pacha aliyemponya mwenzake kwa Kumkumbatia.

Tarehe 17 Oct. 1995, Walizaliwa Watoto mapacha wakike, Brielle na Kyrie, walizaliwa wiki 12 kabla ya tarehe yao ya Kuzaliwa. Kama ilivyo kawaida ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, Walihitaji huduma na uangalifu wa ziada, kila mmoja aliweka katika sehemu yake tofauti zinazotumika kuweka watoto wa namna hii. Kyrie alianza kupata uzito na afya yake ikatulia. Lakini Brielle, alizaliwa na Gram 907 tu, alikuwa na matatizo ya kupumua, matatizo ya moyo na matatizo mengine. Madadkari na Manesi hawakutarajia kama Brielle angeweza kuishi.

Wauguzi wao alifanya kila kitu amabacho waliweza kufanya ili kuboresha afya Brielle, lakini hawakuweza kufanikiwa. Siku moja, mmoja wa Wauguzi aliamua kwenda kinyume cha sheria na masharti ya Hospitali na kuamua kuwaweka Sehemu moja. Aliwaacha watoto na kwenda kulala lakini hakuamini macho aliporudi muda mchache baadae. Kama picha inavyoonekana hapo juu, Brielle alimsogelea dada yake Kyrie, na kumkumbatia kwa kamkono kake kadogo na kumtia moyo. Tangu wakati huo, mfumo wa kupumua wa Kyrie ukarudi kua sawa na afya yake ikaimarika kuanzia hapo.

Karie na Brielle miaka 17 Baadae. (2012)