Tuesday, July 16, 2013

Radi iliyoua Kikosi kizima cha timu ya soka wakiwa uwanjani

Mwaka 1998, huko mjini Kisai nchini Kongo - DRC, Radi ilipiga kwenye kiwanja kimoja cha Soka nchini humo wakati mechi ikiendelea na Kuua kikosi kizima, yaani wachezaji 11 wa timu moja na kuacha wachezaji wote wa timu nyingine wakiwa wazima kabisa.
.
Gazeti la kila siku la Kinshasa,  
L'Avenir liliripoti kuhusiana na maoni ya wananchi na wakazi walio shuhudia tukio hilo na kusema kua wengu wanahusisha tukio hilo na imani za Ushirikina.
.
Wakati Radi hiyo ina piga, timu zote mbili zilikua zimetoshana nguvu na kufungana 1-1 na mechi ilikua ikiendelea. Timu iliyouwawa na radi hiyo ni timu ya wageni 
gazeti la L'Avenir liliripoti pia.




Chanzo: BBC