Bila shaka utakuwa umewahi kuona waendesha baiskeli wa ajabu katika mashindano au mitaani, kadiri teknolojia na uzoefu unavyozidi kuongezeka miaka hii. Ila nina hakika hata kama uliwahi kuona baiskeli inayoweza kutosha kwenye mfuko wa suruali, basi ilikuwa ya kuchezea watoto.
Lakini hii ni halisi, baiskeli yenye pedo ndogo mara tano zaidi ya mguu wa binadamu, imeendeshwa katika mashindano na mtu mzima mrusi (Russian adult), kama baiskeli ya kawaida.
Licha ya udogo wake, baiskeli hiyo imekamilika kabisa; ina matairi, pedo n.k., japo katika ukubwa ni ndogo kuliko kiatu cha mwanadamu
Huenda hili likaonekana kawaida lakini utakubaliana na mimi kuwa inahitaji ujuzi wa ziada kuendesha baiskeli yenye pedo ndogo mara tano kuliko mguu wako