"Upendo hauna mipaka". Msemo huu umethibitishwa kuwa kweli na wanandoa wachanga Arin Andrews na Katie Hill. Wanandoa hao waliokutana miaka miwili kabla ya kuoana kwao, katika kikundi cha kuunga mkono ubadili wa jinsia, na walipendana kutokana na hadithi zao za maisha kufanana
Hapo awali Andrew alikua msichana aliyeitwa Emerald, na Katie alikua mvulana aliyeitwa Luke. Wote wawili waliamua kubadili jinsia baada ya kujiona hawazistahili
Kipindi cha miaka miwili iliyopita kilikuwa kigumu kwa vijana hao, iliwalazimu kuhama shule na kupoteza baadhi ya marafiki, lakini kukutana kwao imekuwa faraja kwao
Andrews anaishukuru familia yake na mkewe Katie kwa kumkubali na kumwonesha upendo. Kwasasa zoezi limekamilika kwa wote wawili, na wanaamini jamii itakubali jinsia zao mpya na changamoto zao zitabaki historia
Picha ya kwanza ni Andrew (kushoto) na Katie (kulia) baada ya kuoana, wakati picha ya pili ni vijana hao wakati wa utoto wao

