
BAMIA
Chukua mbegu za bamia uzikaange, uzisage mpaka ziwe unga.
Chemsha nusu kikombe cha unga huo katika glasi 2 za maji kisha chuja.
Dozi:
Wakubwa kikombe 1 x 3 kwa siku kila baada ya mlo.
Miaka (7-12 ) anywe nusu kikombe x 3 kwa siku kila baada ya mlo. Huruhusiwi kuchemsha na kuweka bali fanya hivyo kila unapotaka kunywa.
Miaka (2-6) robo kikombe x 3 kwa siku.
Kwa watoto wachanga kijiko kikubwa 1 x 3, mpatie baada ya kunyonya au kunywa maziwa na kushiba.

MBEGU ZA PAPAI
Chukua mbegu za papai zikaushe kivulini, baada ya hapo zisage ziwe unga laini.
Dozi:
Weka kijiko kimoja cha chai kwenye uji, kama huwezi kutumia uji unaweza kuweka kwenye chai lakini muhimu sana kwenye uji.
Kwa siku tumia mara tatu.
Kwa mtoto miaka 5-10 unaweza kumgawia nusu ya mtu mzima.
Kwa mtoto wa miaka 3-5 unaweza kumgawia ¼ wote x 3 kutwa.

ALIZETI
Chemsha kilo moja ya majani ya alizeti katika lita 2½ za maji kwa dakika 15. Dozi:
Kunywa nusu glasi x 3 kwa siku, tumia tiba hii kwa muda wa siku 5.
Miaka (7-12) ¼ glasi x 3 kwa siku. Miaka (2-6) kijiko 1 x 3 kwa siku.
Tiba hii ni kwa wale waliotuma ujumbe wakiomba niirudie tena kwani nilishaandika siku za nyuma.
Nashukuru kwa kunisoma, wiki ijayo nitajibu maswali mengine lakini wasomaji nawaomba msome kila toleo kwani maswali mengi yanajirudia.