Kupunguza uzito au unene kunaweza kuwa jambo jema kwa afya yako. Zifuatazo ni njia za asili au za kawaida za kupunguza uzito.
1. Viungo vya chakula
Viungo vinavyotumika katika kutayarisha chakula vinaweza kuwa msaada mkubwa katika kupunguza uzito wa binadamu. Viungo muhimu katika zoezi hilo ni pilipili nyeusi, tangawizi kavu na mdalasini, vyote hivi ni muhimu ukavijumuisha katika mlo wako wa kila siku.
2. Mchaichai
Mchaichai una vionjo vya asili vya kafeine (caffeine), hivyo kunywa vikombe vinne kila siku vya mchaichai kwani husaidia sana kupunguza uzito. Vilevile, epuka kunywa vinywaji baridi na juisi zenye sukari nyingi.
3. Mazoezi unapoamka asubuhi
Unapofungua macho asubuhi, jaribu kukaa bila kutumia mikono yako. Inyooshe miguu yako kwa mbele kisha inama mpaka usikie sauti ya kunyooka kwa mgogo wako na katika uvungu wa magoti. Halafu rudi taratibu mpaka ujilaze tena kitandani. Zoezi hili kusaidia kupunguza nguvu za kemikali za chakula mwilini na kuimarisha mwili wako kwa jumla.
4. Kunywa maji kwa vingi
Kunywa maji mengi kunaimarisha nguvu ya mwili wako katika kujenga au kuvunja kemikali mbalimbali (metabolism) na kurahisisha kusambaza au kunyonywa kwa virutubisho. Maji pia huondoa sumu na takataka mwilini mwako ambazo huzuia ufanyaji kazi mzuri wa kupambana na kemikali.
5. Kula matunda kwa wingi
Matunda ni chanzo kikubwa cha nishati mwilini na yana kemikali chache. Matunda husaidia kupunguza uzito kwani yana vitamini nyingi na virutubisho vingi ambavyo huusaidia mwili wako kuwa katika afya njema.
6. Mazoezi
Bila kufanya mazoezi mwili wako kamwe hauwezi kuwa na afya njema. Mazoezi huondoa kemikali zisizotakiwa mwilini na kukufanya ukawa na afya njema na mwembamba.
7. Fikiri kabla ya kula
Usiwe na tabia ya kula kinachopatikana. Chagua vyakula bora na kula taratibu kwani unapokula chakula kwa kukitafuna vizuri ndivyo mwili wako utakavyovipokea vizuri virutubisho vilivyomo katika chakula.\
8. Shiriki michezo
Kushiriki michezo mbalimbali ni njia muhimu ya kuupa mazoezi mwili wako na kupunguza kemikali zisizotakiwa. Jichangamshe kwa kushiriki michezo au mazoezi katika viwanja au maeneo yaliyo nje ya makazi yako.
9. Punguza matumizi ya chumvi
Matumizi makubwa ya chumvi husababisha unene na kuongezeka kwa shinikizo la damu.
10. Usile karibu na wakati wa kulala
Kuchelewa kula na baadaye kwenda kulala husababisha matatizo. Hivyo, kula mapema ili uupe mwili wako nafasi ya kukichuja vyema chakula. Ukichelewa kula halafu ukaenda kulala unakuwa unazuia mchakato wa kuchujwa vizuri chakula na hivyo kusababisha unene kutokana na kulundikana kwa mafuta mwilini.