Saturday, December 14, 2013

Daktari wa Miaka 7

Akrit Jaswal alizaliwa tarehe 23 Aprili 1993 mjini Nurpur nchini India. Kwa mujibu wa mama yake mzazi, Akrit alianza kuongea akiwa na umri wa miezi kumi (10) tu, alianza kujua kusoma akiwa na umri wa miaka mitano tu. Akrit alianza kuonyesha mapenzi makubwa kwenye kazi ya udaktari akiwa na umri mdogo sana.

Madaktari wa hospitali za maeneo ya nyumbani kwao baada ya kumgundua walianza kumruhusu kuingia kwenye vyumba vya Upasuaji. Akrit alitumia nafasi hiyo vizuri na kujifunda kila kitu alichoweza kujifunza kuhusu upasuaji. Wakati akiwa na Umri wa miaka 7, familia moja masikini iliyoshindwa kulipia matibabu ya binti yao, ilisikia kuhusu Uwezo wa ajabu wa mtoto Akrit Jaswal na wakaamua kumuomba awasidie kumfanyia Uparesheni binti yao. Uparesheni hiyo ilifanyika kwa mafanikio mazuri na kumfanya Akrit kuweka rekodi ya dunia ya kua Daktari wa kwanza kufanya Upasuaji akiwa na miaka 7.