Thursday, January 23, 2014

Mvulana wa miaka 17 aliyekufa kwa ugonjwa wa Kuzeeka

Sam Berns akiwa na Wazazi wake.

Mvulana wa miaka 17 raia wa Israel aliripotiwa kufariki dunia kwa ugonjwa au maradhi ya Uzee, kwa mujibu wa msemaji wa hospitali huko Massachusetts.

Sam Berns, aliyekua mwanafunzi wa “High School” aliugua ugonjwa ujulikanao kwa jina la kitaalam la Progeria ambao ni ugonjwa adimu sana wa “Kuzeeka kabla ya wakati wako”.

Progeria ni ugonjwa wa kimaumbile ambao unahusisha muonekano wa kuzeeka kwa haraka kupita kiasi, hii ni kwa mujibu wa matokeo ya Utafiti uliofanywa kuhusu ugonjwa huo.

Takwimu zinaonyesha kua kwa wastani watoto kati ya 200 na 250 wanaugua ugonjwa wa Progeria duniani kote na huishi wastani wa miaka 13 kabla hawajafa.

Berns aligundulika kua na ugonjwa huu tangu akiwa na umri wa mwaka 1 na miezi 10, na alifariki mnamo tarehe 10. Jan. 2014 akiwa na umri wa miaka 17.