Sunday, January 26, 2014

Abakwa kwa amri ya wazee wa kijiji!

Mnamo tarehe 22 Januari 2014, Genge la wanaume 13 walikamatwa na polisi kwa kosa la Kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 20 katika jimbo la Benghal Magharibi.

Inadaiwa wanaume, hao walimbaka mwanamke huyo kufuatia amri ya wazee wa kijiji ambao wamejipa wenyewe mamlaka ya mahakama ya kitamaduni.Inaarifiwa amri ya kumbaka mwanamke huyo ilitolewa na wazee wa kijiji ambao walipinga uhusiano wake na mwanamume kutoka katika jamii tofauti.

Suala la ubakaji limekuwa likiangaziwa sana nchini India.
Hasira ya mamilioni ya watu iliyotokana na kisa hicho ilipelekea vyombo vya habari nchini India kuanza kuangazia tatizo hilo , swala ambalo wangi walihisi lilikuwa limepuuzwa kwa muda mrefu.

Serikali ya nchini humo nayo ilianza kuweka sheria kali kuhusu dhuluma za kingono dhidi ya wanawake. Lakini utekelezwaji wa sheria hizo bado ni changamoto katika nchi ambayo ustawi wa kijamii unakuwa kwa kujikokota na ukosefu wa usawa likisalia kuwa tatizo jengine kubwa.

Wengi wameshangazwa kuwa katika kisa hiki, ubakaji umeamrishwa na kikundi cha wazee wa kijiji ambao wamejipa mamlaka kama viongozi wa kijamii.

Chanzo: BBC Swahili