MTOTO Nathan Thomson alichomwa kisu usoni na Hugh Clark, wakati akipigania kumwokoa
mama yake dhidi ya mtu huyo aliyekuwa amelewa na aliyekuwa na kisu akitaka kuua. Nathan
alimrukia Clark mgogoni ili asiendelee kumchoma visu mama yake, Ena. Kuona hivyo, Clark
alimgeukia mtoto huyo na kumchoma usoni. Hata hivyo, Nathan alifanikiwa kumwokoa mama yake
ambaye aliishia kumchowa mara nane lakini baadaye akapona. Mtu huyo alikuwa amevunja na
kuingia katika nyumba ya familia hiyo huko Fife, Scotland.