Friday, February 28, 2014
Maajabu, Brauzia hii itafunguka kwa Umpendaye tu!
Wanateknolojia nchini Japani wamegundua Brauzia ambayo itafunguka kwa mtu mwenye mapenzi ya kweli tu.!!
Brauzia hiyo ya "Smart Bra" kama inavojulikana kitaalam ambayo pia imepewa jina la utani la "True Love Tester" yaani Kipimo cha Mapenzi Halisi. Watengenezaji wa bra hiyo wamesema imetengenezwa na Vitambuzi maalumu (Sensors) ambavyo hupima mapigo ya Moyo na viashiria vingine wakati muhusika (Mwanamke) anapokutana na mtu anayetaka kufanya naye mahaba. Kwahiyo kwa kifupi Bra hiyo inagundua Upendo kwa mtazamo wa Kisaikolojia ambao maranyingi hudhaniwa kua ni "Msisimko kwa kimahaba"
Watengenezaji wa bra hiyo, Ravijour wamesema wana uhakika na bidhaa yao hiyo ambayo itakua inafanya kazi kwa ushirikiano na programu ya simu ya mkononi ambayo itakupima kupitia sensors zilizowekwa kwenye bra hiyo na kisha kuamua kuiruhusu bra hiyo kufunguka au la. Wanaongeza na kusema lengo kuu la kutengeneza bra hiyo ni kumwezesha mtumiaji kuweka mipaka dhidi ya watu asiowapenda.
Labels:
Maajabu,
teknolojia,
upendo,
Vituko,
wanawake
