Moyo wa Bandia ambao umekua kwenye maandalizi kwa miaka 75 iliyopita, umepandikizwa kwa mara ya kwanza kwenye kifua cha mzee wa miaka 25 huko Ufaransa. Upasuajia na upandikizaji huo ulifanyika katika hospitali ya Georges Pompidou European Hospital mjini Paris, Ufaransa tarehe 18. Des. 2013
Moyo huo wenye uzito wa kilo 0.9 unatarajiwa kumwezesha mtu huyo kuishi nao kwa muda wa miaka 5, wakati na kupa uwezo wa kufanya mambo yote ambayo hakuweza kuyafanya wakati akiwa na matatizo ya moyo wake wa kawaida.
Gharama za Moyo huo wa bandia ni kiasi cha Dola za Marekani 246,000 ambayo ni sawa na zaidi ya Shilingi Mil. 390 za Tanzania.
Hata hivyo wataalamu wanasema lengo kubwa la moyo huo ni kumwezesha mgojwa kushi kwa angalau miaka 5 wakati akisubiria kupatikana moyo halisia kutoka kwa wachangiaji (Donors).