Mwaka 2009, Bwana Le Van alishika vichwa vingi vya Habari nchini Vietnam baada ya kugundulika kua amekua akilala na maiti ya Mke wake kwa miaka mitano. Miaka miwili badae, waandishi wa gazeti la Nguoi Lao Dong walifanya utafiti tena na kugundua kwamba mtu huyo bado anaendelea kulala na maiti hiyo ya mkewe na Mmlaka ya nchi hiyo haikua na lakufanya ili kumzuia kufanya hivyo.
Magazeti nchini Vietnam yamekua yakiendelea kutoa picha za Le Van akiwa amelala na mdoli ambao kwa ndani una mabaki ya mwili wa mkewe. Bwana Le Van anasema mke wake alipofariki alishindwa kukubaliana na hali ya kumpoteza mpenzi wake, ndipo akaamua kuendelea kulala naye kitanda kimoja. Miezi kadhaa baadae baabda ya mwili huo kuharibika zaidi, bwana huyo aliamua kuchonga mdoli na kuweka mabaki na mkwe ndani yake na kisha kuendelea kulala naye.
