Saturday, March 8, 2014
Jinsi ya kupambana na tatizo la Harufu mbaya ya Kinywa
Harufu mbaya ya mdomo ni moja kati ya matatizo ambayo yanaweza kumpata mtu yeyote yule kwa urahisi sana. Chanzo cha tatizo hili maranyingi ni aina ya vyakula tunavyokula au mara nyingine ni matatizo ya kiafya ambayo hujulikana kitaalam kwa jina la Halitosis. Kitu kibaya zaidi kuhusu tatizo hili ni kwamba ni rahisi zaidi kupata tatizo hili kuliko kulitibu. Lakini pamoja na hayo zipo njia rahisi na sahihi za kukabiliana na tatizo hili:
1. Safisha kinywa vizuri:
Maelfu kwa maelfu ya bakteria hupenda sana kukaa kwenye vinywa vyetu. Kwa kulitambua hilo ni muhimu sana kuweka vinywa vyetu safi kila saa ili kupambana na bakteria hao. Kwa kadri unavyo safisha kinywa chako mara nyingi ndivyo unakiweka salama dhidi ya bakteria hawa ambao ndio chanzo kikubwa cha harufu mbaya ya kinywa. Inashauriwa kushafisha kinywa vizuri kwa kutumia dawa angalau mara 2 kwa siku.
2. Kunywa maji kabla ya Kulala usiku.
Wataalam wanasema maranyingi harufu mbaya ya mdomo hutokea wakati kinywa kinapokua kikavu. Wakati wa usiku tunapokua tumelala mwili hutengeneza kiasi kidogo zaidi cha mate ukilinganisha na wakati wa mchana tunapokula na kunywa. Pia kitaalam mate huwa yanakua na hewa ya Oksijeni, ambayo hupunguza kuzaliana kwa bakteria. Kwa maana hiyo basi unapokunywa maji kabla ya kulala unauwezesha mwili wako kuzalisha mate mengi zaidi wakati umelala ili kusaidia kinywa kupambana na bakteria wanaoleta harufu mbaya ya kinywa.
3. Vyakula tunavyokula:
Kuna vyakula ambavyo vinaweza kuathiri harufu ya kinywa chako kwa namna moja au nyingine. Hivyo basi kama wewe ni moja kati watu wanaosumbuliwa na tatizo hili, inabidi uanze kuchunguza aina za vyakula unavyokula hasa wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala. Vitunguu maji na vitunguu maji ni moja kati ya vyakula hivyo. Kwa ujumla Vyakula ambavyo vina kiasi kikubwa cha protini na kiwango kidogo cha wanga ndivyo vyakula vinavyoweza kusababisha tatizo la kunuka mdomo. Baadhi ya vyakula hivi ni Mayai, Maharagwe, karanga nk.
Labels:
afya,
dawa,
dondoo,
tiba asilia,
vyakula
