Wednesday, March 5, 2014

Kwa wanaotumia Choo cha Kukaa: Jinsi na kujiepusha na kurukiwa majimachafu wakiwa wanapata Haja kubwa.

Kama utatumia choo cha kukaa lazima utakua uliwahi kusumbuliwa au kuchukizwa na kitendo cha Kurukiwa na maji (ya chooni) pindi unapokua unajisaidia Haja kubwa. Hata mimi imenisumbua kwa muda mrefu sana lakini leo nimelipatia ufumbuzi jambo hili, na hii ndo jinsi ya kukabiliana nalo:

1. Kata kipande cha Karatasi ya Chooni (Toilet paper).

2. Tumbukiza karatasi hiyo kwenye tundu la choo chako cha kukaa (kwenye maji), kama inavooneka kwenye picha hapo juu.

3. Sasa unaweza kufurahia huduma ya Hajakubwa (kukata gogo) bila ya kuhofia kurukiwa na maji machafu ya chooni.