Saturday, March 15, 2014

Maajabu ya Mungu: Samaki anayepaa kama ndege!


Samaki wapaao wapo kwenye bahari zote. Lakini watafiti wanasema kua aina hii ya samaki hupatikana zaidi katika bahari zilizopo katika ukanda wa Tropical. Samaki hao wenye mapezi (fins) makubwa zaidi ukilinganisa na aina nyingine, ambanyo ndiyo humwezesha kupaa kwa mita kadhaa juu ya uso wa maji ili kujiepusha na maadui zake. Watafiti wanasema samaki hao wana uwezo wa kupaa kwa umbali hadi wa mita 50 kwa wakati mmoja.