Mambo ya Kuzingatia ukitaka kuishi Maisha ya Furaha
AFYA:
- Kunywa maji mengi
- Kula zaidi vyakula vinavyotokana na Miti au Mimea
- Cheza michezo
- Soma vitabu zaidi
- Tafuta muda ya kuakaa kimya pekeyako angalau dakika 10 kwa siku
- Lala kwa masaa 7 hadi 8 kwa siku.
- Tumia dakika 10-30 kutembea kila siku. Tabasamu wakati unatembea
UTU:
- Usilinganishe maisha yako na ya mtu mwingine.
- Epuka mawazo maovu au mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako. Badala yake tumia zaidi nguvu zako kwenye mambo chanya.
- Usifanye jambo lolote kupita kiasi. Kuwa na mipaka
- Usipoteze mda wako kuwasema wengine (Umbea)
- Ota zaidi wakati uko macho.
- Sahau kuhusu mabaya ya yaliyopita. Usimkumbushe mwenza wako kuhusu makosa yake ya zamani.
- Maisha ni mafupi, usipoteze mda wako kumchukia mtu yeyote.
- Hasira na Machungu ni Jela, usikubali kujifunga, jifunze kuachilia.
- Usiruhusu mtu mwingine awe sababu pekee ya furaha yako.
- Tambua ya kwamba maisha ni Shule na upo kwajili ya kujifunza. Matatizo ni kama topic tu fulani ambayo huja na kupita, lakini kile unachojifunza kitadumu daima.
- Tabasamu na Cheka zaidi
- Sio lazima ushinde kila ubishi, Kubali kushindwa wakati mwingine.
JAMII:
- Wapigie simu watu wa familia yako kila mara
- Kila siku jaribu kuwapa wengine kitu kizuri.
- Samehe kila mtu kwa kila kitu.
- Tumia muda kuwa karibu na watu wenye umri wa zaidi ya miaka 70 na wenye umri chini ya miaka 6.
- Jaribu kufurahisha watu angalau watatu kila siku.
- Usijisumbue na kile watu wanasema kuhusu wewe, kuna mambo ya muhimu zaidi kufanya.
- Kazi yako haitoweza kukuhudumia siku unaumwa lakini marafiki wanaweza. Kazi isikufanye kuwasahau marafiki.
MAISHA:
- Fanya jambo jema!
- Kama jambo halina Manufaa, achana nalo.
- Hata kama hali ni Mbaya au Nzuri kiasi gani, lazima itabadilika.
- Hata kama unajiskiaje, kumbuka kuvaa vizuri na kusafisha kinywa.
- Hata ushindi mdogo ni ushindi.
- Mazuri zaidi bado yanakuja
- Kua makini kwa yale unayosema kwa Watoto.
- Kua makini na maneno unayojinenea.