Tuesday, December 31, 2013

Mtoto aliyeokolewa kwenye bomba la chooni na kupona.

Mama mmoja ambaye jina lake halikujulikana, aliambia polisi kuwa alijifungua mwanawe akiwa chooni na kuwa mtoto huyo aliteleza na kuanguka ndani ya bomba hilo kwa bahati mbaya.


Mama huyo anaripotiwa kuangua kilio cha mwanawe , licha ya kuwa hakukubali kuwa ni mwanawe hadi baadaye.


Mtoto huyo alopokea matibabu hospitalini baada ya kuokolewa kutoka ndani ya bomba la maji taka. Bomba hilo lilikatwa kwa ustadi baada ya majirani kusikilia kilio cha mtoto huyo mjini Jinhua.


mtoto hospitali

Mama huyo aliongeza na kusema kuwa alijaribu kumzuia mtoto wake kuanguka baada ya kujifungua kwa ajali akiwa hospitalini lakini alianguka ndani ya bomba. Hata hivyo alimweleza mpangaji wake kulingana na shirika la habari la Xinhua.


Mama huyo alisema hakuwa na uwezo wa kumlea mwanawe kwa hivyo hakuambia yeyote kuwa ni mwanawe. Hata hivyo baadaye alijitambulisha na kuambia polisi ni mwanawe baada ya kuokolewa kwake.


 

Kisa hicho kimezua mjadala mkali kwenye mitandao ya China huku baadhi wakisema kuwa mtoto huyo alikuwa ametupwa na mamake kwa maksudi.


Sheria za China za kupanga uzazi ni kali mno huku familia ikiruhisiwa kuzaa mtoto mmoja pekee na wazazi wanaweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini ikiwa watapatikana na hatia ya kupata zaidi ya mtoto mmoja.


 Chanzo: BBC Swahili