Amber Miller alikuwa na ujauzito wa karibu wiki 39 na alikuwa akitarajia kupata mtoto wa
pili siku yoyote wakati alipoanza kukimbia katika mashindano ya mbio ndefu (marathon) huko
Chicago, Marekani. Mwanamke huyo alikimbia na wakati mwingien akatembea licha ya
kwamba alianza kusikia misukosuko ya kiumbe kilichokuwa tumboni mwake wakati anaelekea
kumaliza mbio hizo. Hata hivyo, Miller aliweza kumaliza mbio hizo kabla ya muda mfupi
baadaye kujifungua mtoto wa kiume.
‘Mama’ huyo alimaliza mbio hizo kwa kutumia saa 6, dakika 25 na sekunde 50!