Wednesday, January 8, 2014

Msichana ajifungua wakati akicheza ‘kickboxing’

PAMELA VUGTS mwenye umri wa miaka 17 na mwenyeji wa Den Bosch, Uholanzi,

alikimbizwa hospitali muda mfupi baada ya kushiriki mpambano wa ngumi na mateke

(kickboxing) na kujikuta akijifungua kichanga cha kike. Bila ya yeye na mpianzani wake kujua

alikuwa mjamzito, Pamela kumbe alikuwa na ujauzito wa miezi saba wakati akiingia ulingoni.

Lakini alipopigwa teke tumboni, msichana huyo alianza kuvuja damu na hivyo kukimbizwa

hospitali.

Baada ya tukio hilo, baba yake alisema: “Msichana huyu alionekana kuwa ameongezeka unene

kidogo, lakini kwa vile alikuwa anakwenda katika siku zake kama kawaida tuliona kwamba

aliongezeka uzito kwa vile alikuwa katika mapumziko.”