Video hii iliwekwa mtandaoni Jumapili ya tarehe 12 Mei 2013 ikionyesha Abu Sakkar, kiongozi wa Kikundi cha Waasi cha Farouq Brigade nchini Syria akila Moyo wa mmoja wa wanajeshi wa jeshi la nchi hiyo.
Sakkar alionekana akipasua kiwiliwili cha Askari huyo huku akisema “Naapia kwa mungu tutaendelea kula Mioyo na Maini yenu nyie Askari wa huyu mbwa, Bashar.” Huku wenzake wakifurahia na kusema “Allahu akbar”